
Aidha Mkurugenzi wa Msama Promotion Bwana Alex Msama alieleza kuwa Mh.Bernard Membe waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa atakuwa Mgeni rasmi.Wengine ni wakuu mbalimali wa serikali,wafanya biashara na wengine wengi.
Rose Muhando anatarajia kushirikiana na wasanii mbali mbali wa muziki Maryanne Tutuma na Anastazia Mukubwa wa Kenya.Kwa upande wa Tanzania ni Christina Shusho,Upendo Nkone,Upendo Kilahilo,Atosha Kissava,Ephraim Sekeleti,Glorious Celebration Group,Kinindoni Revival Choir na vile vile Faraja Ntaboba kutoka Jamuhuli ya Kidemokrasia ya Kongo
"Kuna wasanii wengi ambao wamekubali kuungana kushiriki kwenye hiyo shoo"Alieleza Msama
Kiingilio itakuwa 2000/- kwa mtoto,5000/- kwa wakubwa na 10,000/- kwa viti maalumu
No comments:
Post a Comment