Muda si mrefu maeneo ya round about ya barabara ya Sam Nujoma ali maarufu kama round about ya mlimani City.Roli limeanguka likiwa linakata kona kuelekea njia ya chuo kikuu cha Dar Es Salaam mishale ya saa sita kasoro asubuhi likiwa limebeba tenki la maji,ambapo ilisababisha msongamano wa magari kwa muda huo mfupi.Huku askari wa usalama barabarani akiwa tayari kashawasili na gari la kuvutia magari ali maarufu kama break down.
Trafiki akiwa anafanya kazi yake pale
Break Down zikiwa tayari kwa kazi,Kinachoshangaza kuhusu hawa watu sijui huwa wanapata habari wapi maana ajali ikitokea tuu,ndani ya dakika ikadhaa wameshawasili.
Gari ikiwa inawekwa sawa,nao wananchi hawakuwa mbali kushuhudia tukio hilo.
Eneo hilo lilitapakaa mafuta na maji kama inavyoonekana kwenye picha
No comments:
Post a Comment