
Aidha alieleza wabunge wa CCM watakutana tarehe 3 Aprili kuchagua wagombea 24."Wabunge watakao chaguliwa watapigiwa kura na bunge la Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania,CCM wakiwa na nafasi nane"
Aliongezea kuwa watano kati ya nane watatoka bara na watatu watatoka Zanzibari.Nafasi za wanawake zikiwepo tatu, moja ikitoka Zanzibari.
Nape Nnauye,Abdulrahman Kinana na Dogo Mabrouk ndio waliochaguliwa kusimamia uchaguzi huo wa Aprili (3)Tatu.Bara walipendekeza wanawake 17 na wakachaguliwa 12,wanaume wakiwa 45 na kuchaguliwa 17 tuu.Na kwa upande wa visiwani walipendekeza wanawake 8 na kuchaguliwa 5 na wanaume 8 ambao walichaguliwa wote.
Wengi ya waliochaguliwa kugombea nafasi hiyo mwaka jana hawakufanikiwa wakiwemo Shy-Rose Bhanji,Siraju Juma Kaboyonga,Ruth Blasio Msafili na wengine wengi wakiwemo na watoto na ndugu wa wanasiasa wakongwe akiwemo Charlse Makorongo Nyerere.
No comments:
Post a Comment