Mkutano wa umoja wa nchi za Africa mashariki umejadili kuondoka kodi zinazotozwa na serikali ya Tanzania juu ya maroli yanayotoka Kenya.Mamlaka ya kodi ya Tanzania imekuwa ikitoza ushuru wa dola 200 kwenye maroli yanayoingia nchini,jambo hilo limekuwa kikwazo kwa wafanya biashara wa Kenya wanaoleta bidhaa za nchini Tanzania.
Ingawa haikueleweka kuwa mkutano huo ulizungumzia pia na kodi inayotozwa kwenye magari ya utalii yanayoingia Tanzania.Alhamisi iliyopita waziri Najib Balala alilalamikia kuingia kwa mizigo kinyume cha sheria inayobebwa na magari ya watalii ambayo inanunuliwa na viwanda vya ndani
Aidha Waziri Sirma alieleza Kenya itapunguza vizuizi vya barabara kutoka 36 mpaka 5 na Tanzania 30 mpaka 15 wakati Uganda,Burundi na Rwanda hapatakuwa na mabadiliko.Wingi wa vizuizi hivyo vinachangia kuchekewa kwa mizigo ndani ya jumuiya,kuongezeka kwa gharama vilevile na uwepo wa rushwa.
TBS Kanda ya Mashariki Yateketeza Tani 64 za Vipodozi Vyenye Viambata sumu
-
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) kupitia ofisi ya Kanda ya Mashariki
limekamata na kuteketeza tani 64 za vipodozi vyenye thamani ya takribani
Shilingi mil...
10 hours ago
No comments:
Post a Comment