Ilikuwa ni baada ya kutoa kadi nyekundu mbili kwa Haruna Niyonzima na Nadir Haroub.Yanga ilijikuta kumaliza mchezo huo na wachezaji nane huku ikipoteza mechi kwa kufungwa 3-1
Aidha kamati ya ligi kuu iliamua kumfungia kucheza soka kipindi cha mwaka mzima na mchezaji huyo kukiri kosa na kukubali adhabu ingawa mpaka sasa hajakabidhiwa barua yoyote
Naye, Jerryson Tegete aliyefungiwa mechi sita pamoja na adhabu ya faini ya sh.500,000 aidha alijitetea kwa kusema aliingia uwanjani kwa nia ya kutuliza zengwe na sio vinginevyo.Mbali na mchezaji huyo adhabu hiyo pia iliipita kwa Nadir Haroub, ambaye atakosa mechi sita pamoja na adhabu ya kulipa faini ya Sh500,000, huku Omega Seme na Nurdin Bakari wakikosa mechi tatu na kulipa faini ya Sh500,000.
Kwa upande wa msemaji wa Yanga, Luis Sendeu kwa niaba ya uongozi alisema, wamepata barua toka TFF, lakini hawajaridhishwa na uamuzi huo kwani haukuzingatia kanuni za uendeshaji ligi
Kwa upande wa msemaji wa Yanga, Luis Sendeu kwa niaba ya uongozi alisema, wamepata barua toka TFF, lakini hawajaridhishwa na uamuzi huo kwani haukuzingatia kanuni za uendeshaji ligi
No comments:
Post a Comment