Wanafunzi wa chuo kikuu cha Afya na Sayansi kishirikishi muhimbili(MUHAS) walalamikia kukaa njaa kwa zaidi ya siku tano chuoni hapo
Ambapo uongozi wa chuo hicho ulikiri kutokuwepo kwa chakula chuoni humo kwa zaidi ya siku tano,ikawalazimu wanafunzi hao kuandamana moja kwa moja na Mkurugenzi mpaka wizara ya Afya na Ustawi wa jamii na kutaka suluhu dhidi ya adha hiyo.Wengi wao walishauri serikali iwe inawapatia hela ya chakula badala ya chakula hicho kuwa kinatolewa humo chuoni,Aidha,wamelalamika kuwa imewabidi watumie pesa zao za shughuli nyingine na kujigharamikia kwenye chakula.
No comments:
Post a Comment