Photobucket

Monday, April 2, 2012

Chadema yaibuka kidedea,Uchaguzi wa Ubunge Arumeru

Jana tarehe 1 Aprili kulikuwa na Uchaguzi mdogo,kwenye jimbo la Arumeru Mashariki.Vyama mbalimbali vilishiriki ikiwemo Chama cha Mapinduzi(CCM),Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), DP,NRA,UPDP,TLP na SAU.
Vyama vilivyokuwa na Upinzani mkubwa ilikuwa CCM na Chadema,Huku CCM ikimsimamisha Bwn Sioi Sumari na Chadema ikimsimamisha Joshua Nasari(Mh).Uchaguzi ulianza asubuhi kama ilivyooada na kuisha muda wa saa kumi jioni.Baada ya hapo wananchi walitakiwa kuondoka maeneo ya kuhesabia kura,ambayo yalikuwa ya kupigia kura kabla ya hapo.Au kukaa umbali wa mita si chini ya mia moja.
Aidha kwa mujibu wa Bwn Kaghezi zaidi ya watu 120,000 walijiandikisha na ni 60,696 ya wapiga kura waliojitokeza kupiga kura 60,038 ya kura hizo zilikuwa halali
Kulikuwa na vurugu maeneo tofauti tofauti jimboni humo,wengi wao wakiwa ni vijana.lengo lilikuwa ni shahuku ya kutaka kujua matokeo ya Uchaguzi huo,Na matokeo yalikuwa kama ifuatavyo
Imepangwa kutokana na Idadi ya kura walizopigiwa
  1. Chadema- Kura 32,972
  2. CCM- kura 26,757
  3. AFP- kura 139
  4. DP- kura 77
  5. NRA- kura 35
  6. SAU- kura 22
  7. UPDP -kura 18
  8. TLP- kura 18
Kwa matokeo hayo iliifanya Chadema kuibuka Mshindi kwenye Uchaguzi huo kwa Mgombea wao Mh.Jushua Nassari,Hapo ikamfanya Mh.Freeman Mboye mwenyekiti wa Chadema kuitisha mkutano kuwashukuru wananchi kwa kuwaamini na kuwapa ridhaa ya kuongoza jimbo hilo.
Huko Mwanza napo,Chadema yaibuka mshindi kwenye uchaguzi mdogo wa Udiwani kata ya Kirumba.
Msimamizai wa Uchaguzi huo Bwn Aloyce Mkono,ametangaza mgombea wa chadema Mh.Danny Mhangu kwa kura 2938,dhidi ya mgombea wa CCM Mh.Daniel Masamaki aliyepata kura 2131

No comments:

Post a Comment