Nafasi zinazotakiwa za uwakilishi wa Bunge la Afrika Mashariki ni Tisa na CCm imechukua nafasi nane na kuacha nafasi moja kwa vyama pinzani.Asilimia kubwa ya wabunnge Jamuhuri ya Muungano la Tanzania,imekubaliana na hoja ya Chadema kuhairishwa kwa uchaguzi wa wawakilishi wa bunge la Afrika Mashariki.
Chadema ilimuandikia barua Dkt.Thomas Kashililah msimamizi wa Uchaguzi wa wawakilishi wa Bunge la Afrika Mashariki kuhairisha zoezi hilo litakalofanyika kesho.
Nia ni kupitia upya utaratibu wa kuwachagua wabunge watakao enda kuwakilisha Bunge la Afrika Mashariki.
Aidha Bwn. George Simbachawene(CCM) alieleza kuwa haoni haja ya kukataa kuwa kunahitaji mabadiliko,kuna haja ya kuangalia upya kanuni hizo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wabunge wa chama pinzani ukifananisha wa wakati uliopita.
Aidha kada mwengine wa CCM alieleza mfumo wa sasa hauupi nafasi wabunge waliochaguliwa na wanachi wa Tanzania kushiriki katika maamuzi ya uchaguzi huo.Aliongezea pia kama wao wabunge wachache waliochaguliwa na wananchi waliowengi kuwawakilisha,kwanini wawakilishi hao walio wachache wasiwawakilishe wananchi hao kwenye uchaguzi wa Ubunge wa Afrika Mashariki
Aidha Mwanasheria Mkuu mstaafu Andrew Chenge alikatalia mbali hoja hiyo ya Chadema kutaka kuhairishwa kwa Uchaguzi wa wawakilishi wa Bunge la Afrika Mashariki akileleza kwamba haelewi ni kwanini watu wanataka kuongezeka kwa wawakilishi upande wa upinzani,ni haswa haswa kwa mantiki gani aliuliza.Wanataka idadi iongeezeke mpaka ngapi na kwasababu gani aliongezea,aliyasema hayo kwenye mahojianao na Citizen
UFANYAJI WA MITIHANI YA 29 YA PSPTB WAKAMILIKA
-
Bodi ya wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imeendesha mitihani yake ya 29
kwa jumla ya watahiniwa 1,223 katika ngazi za Professonal Diploma, Graduate
...
1 hour ago
No comments:
Post a Comment