Jana tarehe alhamisi ya tarehe 5 ya mwezi Aprili 2012,Jaji Gabriel Rwakibarila, alimvua ubunge Lema katika hukumu ya kesi iliyokuwa ikimkabili kwa kutoa lugha ya kashfa na udhalilishaji dhidi ya aliyekuwa mpinzani wake katika uchaguzi huo wa mwaka 2010, Dk Batilda Burian.
Makosa aliyokuwa akituhumiwa Lema
1)Lema alitiwa hatiani kwa kudaiwa kusema kuwa Dk Burian hakustahili kuchaguliwa kuwa mbunge kwa sababu mila na desturi za makabila ya Waarusha (Wamaasai na Wachaga), mwanamke hawezi kuongoza wazee.
2)Lema kutoa maneno ya kashfa dhidi ya Dk Burian kuwa ni mwanamke asiye mwaminifu, aliyezaa nje ya ndoa na alikuwa na mimba nyingine na bwana huyo aliyezaa naye ambaye siyo mumewe.
3)Lema alifanya ubaguzi wa kidini kwa kusema kuwa Dk.Burian kuwa ni mfuasi wa Al Qaida na hiyo ni sababu anavaa kilemba
4)Lema asihi wananchi kutomchagua Dk.Burian kwa kuuwa hakuwa mkazi wa Arusha kwa kuwa anaishi huko Zanzibar
Aidha Jaji alitupia alitupia mbali mashtaka mawili kati ya manne yaliyokuwa yanamkabiri,Moja ni kuwataka wapiga kura wa Arusha kujihadhari na wanaovaa vitambaa na hijabu wasije kujikuta wanachagua Al Qaida kuwa haihusiani na dini ya Kiislamu.
“Mwanamke kuvaa kitambaa kichwani haina uhusiano wowote na dini ya
Kiislam wala Al Qaida kwani ni dhahiri wanawake wengi ambao baadhi yao
siyo Waislam wanavaa vitambaa. Kwanza ni heshima kwa wanawake kuvaa vilemba hivyo madai haya nayatupilia mbali,” alisema Jaji Rwakibarila katika hukumu yake.
Kuhusu tofauti ya ukaazi kati ya Lema na Dk Burian aliyedaiwa kuolewa
na kuishi Zanzibar, Jaji huyo alisema hoja hiyo isingeharibu wala kwenda
kinyume na maadili ya kampeni kwani kisheria Mtanzania ana haki ya
kuishi upande wowote wa Jamhuri ya Muungano, yaani Bara na Visiwani.
Aidha alimtaka Lema kulipia gharama zote za kesi hiyo.Kama hajaridhika na hukumu hiyo anaruhusiwa kukata rufaa,Jambo ambalo Lema hakukubaliana nalo na kueleza yeye si mbunge wa rufaa.
Ni kweli Mahakama ni chombo cha dola,lakini kwa uamuzi waliofanya wa kumvua ubunge,ni haki kwa wananchi waliompigia kura na serikali kwa ujumla???
Kuandaa kwa uchaguzi mwingine ni gharama kubwa,na pesa hizo zingeweza kutumiwa kurekebisha mambo mbalimbali yanayoikabiri nchi yetu.Hususani hali ya uchumi wetu unavyo anguka na wanachi wanazidi kuumia kwa kupanda kwa gharama ya vitu mbalimbali.
Mwananchi wa hali ya chini anaumia sana na mabadiliko haya ya kupanda kwa bei kwa vitu mbalimbali nchini.Imefika wakati viongozi wetu kuachana na mambo ya ushabiki wa vyama na kutumikia wananchi walio wachagua na wanaowalipa kwa kutumia kodi mbalimbali wanazotozwa.
MWENYEKITI WA CCM DKT. SAMIA AONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU CCM TAIFA
DODOMA
-
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 17 Januari 2025, ameongoza
Kikao c...
15 hours ago
No comments:
Post a Comment