Baada ya kipindi cha maswali na majibu,
Taarifa ya Mh.Cheo juu ya matumizi mabaya ya fedha za Uma ikiwemo wizara ya Fedha,Halmashauri za serikali na kuleta mjadala mzito.Vile vile Mh.Kabwe Zitto pia alitoa taarifa yake juu ya ukiritimba unaofanyika kwenye sekta hizo. Mh.Mrema pia katika ripoti yake ataka serikali kutoa adhabu ya kinidhamu na kuitaka serikali kutoa maelezo ya kina kukubali ni kwanini ubadhilifu huu upo na unaendelea.Wabunge mbalimbali walichangia mjadala huo kwa uchungu sana na hii ni baadhi tuu ya wabunge waliochangia
Mh.Joshua Nassari(Mbunge Arumeru Chadema) ashangaa kutokuwepo kwa waziri wa wizara ya fedha na waziri mkuu pia wakati wanajadili kuhusu sekta muhimu zinazowahusu,
Aidha Mheshimiwa Halima Mdee Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya Chadema ataka wabunge kubadilika na kutanguliza uzalendo na kuondoa tofauti zao za kichama.
Vile vile Mh.Godifrey Wiston Zambi(Mbunge Mbozi CCM) alilwalipua watendaji wabovu na wala pesa za wananchi,amtaka Mheshimiwa Raisi kuwawajibisha watendaji hao wabovu,ataja zaidi ya bilioni 6.7 zimetafunwa na watumisha wa Serikali
Aeleza fedha nyingi za serikali takribani bilioni 6.7 zilitumika vibaya na ati serikali bado inafanya uchunguzi,Aidha atoa tahadhari kwa serikali,aeleza hata shangaa kama 2015 CCM ikishindwa wakishinda wamshukuru Mungu,Matumizi mabaya bilioni 59,ikiwemo wizara ya Uvuvi 320 Mambo ya nje 215m zimetumika bila taarifa,
Mh.Ali Kessy(CCM) alitaka hotuba zote zirekodiwe raisi asikilize vyote na apunguze upole,Takukuru hawana kazi katika nchi hii wanakamata tuu wezi wa kuku wanakula rushwa,TBS wanaingiza mbolea feki,mafuta feki,waziri amtetea mkurugenzi wa TBS na katibu wake wanafaa waondoke,Alieleza
Aliongezea kuhusu kuwepo kwa misafara ya magari mengi ya mawaziri nia ni kumtisha nani?Aliuliza
Aliongezea hii ni zaidi ya kuwaumiza wananchi,mtumishi wa halmashauri amekuwa na pesa kuliko halmashauri yao,aeleza tunaelekea kubaya,apatwa na usingizi baada ya kuona kila wizara inashoti alimueleza Mzee mapesa(Mh.Cheo)
Msamaha wa kodi na kuuziwa mashamba mikataba yote iangaliwe upya,serikali iwaonee huruma wananchi hawana chakula hawana madawa,awatetea vijana,bilioni 23 zapotea aeleza mbaya ni katibu mkuu wizara ya biashara ataka achunguzwe mali zake,awataka mafisadi na wezi wote wanyongwe ataka bunge liwe la kazi na sio kupigiana makofi.Aidha aeleza watumishi hewa wapo kiwila,shirika la ndege,shirika la reli kigoma n.k
Ataka katibu anyongwe hata kesho, vile vile serikali iangalie pia na kudhamini watu wanaodhaminila na kutaka wabunge wawe wakali katika hili.
Mh.Amina abdallah Amour(Viti maalum CUF) sekta ya huduma shughuli za maendeleo,waziri aliahidi kuwashughulikia lakini mpaka leo bado hajafanya kazi hiyo,kiwango cha misamaa ya kodi holela imefikia asilimia kumi nane ya bajeti ya nchi,aitaka serikali ipitie tena,alaani vitendo vinavyofanyika kwenye halmashauri.
MhPeter Selukamba(CCM) ataka wabunge wasilalamike hivyo wabunge wachukue hatua kwa kutumia kanuni inabidi wafukuze mmoja hadi mwingine ndio watafanya kazi,tunalipa madeni na kuacha kufanya miradi,aelezea hii ni EPA zaidi Ya EPA,vile vile aeleza serikali imedharau bunge hilo, asema Mungu ndiye anayejua huko kulivyo,ataka wabunge wa CCM wafanye kikao cha Chama ataka wamsaidie Raisi kuondoa mawaziri wasiofaa.na wabunge wasiwe sehemu ya kupiga kelele tuu,1.3 trilioni zimetumika na waziri wa fedha bila ya kutaarifu Bunge.
Mh.Felista Bula aliongezea sio kalalamika matumizi mabaya huku watu wanakula nchi na ni kwanini wanateuliwa na sio kufanya usahili,wanafanya makosa na wanabaki kuhamishwa tu,ameshangazwa na ripoti ya kamati ya Mh Cheo kuna deni la trilioni 14.4 zaidi ya bajeti iliyopitishwa mwaka jana deni linakuwa kwa asilimia 39.5 huku uchumi unakuwa kwa asilimia 6.5 aeleza waache kuwadanganya wananchi,sheria yataka mwisho wakutoa dhamana ni asilimia 70 na mpaka sasa na zaidi ya asilimia 90,Mashirika yanaotakiwa kutoka gawio kwa serikali imepungua kutoka bilioni 40 mpaka 28.7
Msd dawa zinakaa siku 21 na wananchi wanakosa dawa,kuomba dawa wizara ya ya afya dawa ziharibiwe ni miezi sita,MSD kupata pesa za kuagiza dawa ni miezi sita hadi tisa na pesa zinapeleka Novemba,Je dawa hizo zitafika lini kwa watumiaji wa Tanzania Aliuliza.
Alilaumu wizara ya fedha kukwamisha maendeleo, mpaka mwezi wa tano 2010 wizara ya Nishati ndio ilipelekewa fedha kwa mara ya kwanza.
Alisema serikali inachukiwa kwa sababu ya watumishi
Lukuvi amtetea waziri na waziri mkuu yeye yupo ndani ya bunge na waziri yupo nje ya nchi kikazi Washinton maandalizi ya bajeti bajeti
Zito ataka ufafanuzi kwa Mnadhimu Mkuu Mh.Lukuvi ni kwanini waziri husika hayupo bungeni.Akaongezea hakuna waziri anayeongoza kusafiri kama wizara ya Fedha ambazo kashfa hizo Mh.Lukuvi alizikana na Mh. Zitto aliongezea ni wizara yenye matatizo sababu ni kutokana hayupo Ofisini muda mwingi
Lukuvi,arudia Mh.yupo washington kwenye kikao na kalenda ya IMF na World bank kuwa huu ndio wakati wake na hawataweza kumsubiria amefatana na naibu waziri wa maji kufuatilia maswala ya maji,apingana.
Aidha Naibu wa Spika aliwataka mawaziri wawe wanatoa taarifa kwenye Bunge ili wabunge wasiwe na taswira tafauti tofauti juu ya kutokuwepo kwao.Ilimlazimu Naibu Spika kuhairisha Bunge mida ya saa Moja Kasoro usiku na Bunge hilo kuendelea Kesho.Muswada huo utajadiliwa kwa muda wa siku mbili.
KARATU YAFIKIWA NA ELIMU YA FEDHA
-
Na. Saidina Msangi, WF, Karatu, Arusha
Wananchi wa Wilaya ya Karatu jijini Arusha, wametakiwa kuhakikisha kuwa
wanatumia Taasisi za fedha zilizosajiliwa am...
3 hours ago
No comments:
Post a Comment