Muda si mrefu jioni hii mishale ya saa moja na dakika ishirini Mheshimiwa Zitto alitoa hoja Bungeni kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu na kukawa na kitabu ambacho wabunge iliwataka kusign ili kubaliana na hoja hiyo na mpaka Bunge linahairishwa ilikuwa ni wabunge zaidi ya sitini waliokuwa wametia sahihi zao.
Aidha Spika wa Bunge Mh.Anne Makinda alitupilia mbali hoja hiyo ya Mheshimiwa Zitto kwa kutumia kanuni za Bunge na Katiba ya Nchi kwa kusudio la kumuondoa waziri mkuu kwa kupiga kura ya utokuwa na Imani naye ilipaswa kuandikwa taarifa ya maandishi inayopaswa kufika kwake kabla ya siku 14 ya siku husika.
Aidha baada ya Mh.Mnyika Mbunge wa Ubungo kusoma muongozo wa spika na kutaja Idadi ya walio tia sahihi kwenye kitabu na kumtaka kwa Idadi hiyo ya wabunge,Na kuuliza Je,Ingewezekana kwa Bunge hilo kujadili swala hilo ifikapo Jumatatu ya wiki Ijayo Tarehe 23.
Ambapo Spika wa Bunge Mh. Anne Makinda aliendelea na msimamo wake huo huo na kuongezea kusema kipindi cha Bunge kitaisha Jumatatu ya Tarehe 23 na kwasababu haijafikia siku 14 hilo swala halitajadilika.
DKT NCHIMBI AAHIDI NEEMA NEWALA | CCM KUONGEZA RUZUKU KWENYE MBOLEA NA
MBEGU KWA WAKULIMA
-
Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia
CCM, Dkt .Emmanuel John Nchimbi amesema miaka mitano inayokuja Serikali ya
Ch...
1 hour ago
No comments:
Post a Comment