Photobucket

Wednesday, March 28, 2012

Asilimia 13 ya wanafunzi wanaoingia kidato cha Tano yapungua

Jumla ya wanafunzi 31,516 kati ya 32,610 ya wanafunzi waliofaulu mtihani wa kidato cha tano mwaka jana ndio waliochaguliwa kuendelea kidato cha tano kwenye shule za serikali na vyuo vya kiufundi
Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi Mh Phillip Mulugo alieleza kuwa kumepungua kwa asilimia 13.34 kwa wanafunzi waliochaguliwa kulinganisha na wa mwaka jana
"Serikali ilitoa jumla ya nafasi 41,000,wavulana wakiwa 15000 na wasichana 26000,lakini ni 9378 ya wasichana na 22138 ya wavulana tuu,ndio waliochaguliwa na kuacha nafasi 9484 zikiwa wazi" Alieleza
Aidha alitoa ujumbe kwa wanafunzi waliochaguliwa na shule za serikali na tayari wameshaingia kwenye shule nyingine,kuwasiliana na wakuu wa shule walizochaguliwa na kwa wanafunzi waliofungiwa matokeo yao kwa sababu moja au nyingine watachaguliwa kuingia kwenye shule hizo za serikali kama watakuwa wamekidhi sifa.
Sababu ya kubaki nafasi nyingi kati ya walio faulu na walio chagulia ni kutoendana kwa masomo waliofaulu na michepuo.Wanafunzi 563 wataingia Arusha Technical School(ATS),Dar Es Salaam Institute of Technology(DIT),Mbeya Institute Of Science na Dar Es Salaam Water Demand Management Institute

No comments:

Post a Comment