Rehema Salum mwanafunzi na Straiker wa shule ya sekondari Lord Baden amechaguliwa kuingia kwenye Timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars.Kocha wa timu hiyo bwana Charles Mkwasa alitaja kikosi cha wachezaji 25 wiki iliyipita na mazoezi yalishaanza rasmi.
Rehema hakubahatika kuchaguliwa kwenye chagua la kwanza,Aliitwa jana na benchi la ufundi la timu ya wanawake kwenye mashindano yaliyo jumuisha shule nane jijini Dar Es Salaam
'Mazoezi yatafanyika kwa muda wa siku kumi na wachezaji 20 ndio watakao safiri kwenda Ethiopia' Alieleza Mkwasa.Watakuwepo wachezaji wapya na wazamani,wapya wakiwepo Amina Salum (Lord Baden Secondary School), Ester Mayala (Street Girls) and Upendo Jeremiah (Pangani).
Kikosi kilijumuishaAziza Mwadini (New Generation, Zanzibar), Asha Rashid (Mburahati Queens), Evelyn Senkubo (Mburahati Queens), Fadhila Hamad (Uzuri Queens), Esther Mayala (Street Girls, Mwanza), Fatuma Bashiri (Simba Queens), Fatuma Gotagota (Mburahati Queens), na Fatuma Khatib (Mburahati Queens).
Wengine ni Fatuma Mustafa (Sayari), Fatuma Omari (Sayari), Mwanaidi Khamis (Uzuri Queens) Hanifa Idd (Uzuri Queens), Maimuna Said (JKT), Mwajuma Abdallah (JKT), Mwanahamisi Omari (Mburahati Queens).
Vile vile Rukia Khamis (Sayari), Semeni Abeid (Tanzanite), Mwapewa Mtumwa (Temeke), Siajabu Hassan (Evergreen), Tatu Salum (Makongo Secondary School), Upendo Jeremiah (Pangani, Tanga), Veneranda Mbano (Tanzanite), and Zena Khamis (Mburahati Queens).
Maandalizi Mkutano wa (EAMJA) Yakamilika kwa Asilimia Mia Moja Huku Nchi ya
Uganda Ikiongoza Kwa ushiriki Mkubwa.
-
Na Jane Edward, Arusha
Maandalizi ya Mkutano wa 21 wa Chama cha Majaji na mahakimu (EAMJA)kutoka
Jumuiya ya Afrika Mashariki yamekamilika kwa asilimia...
54 minutes ago
No comments:
Post a Comment