Photobucket

Tuesday, March 20, 2012

Kivukoni is stinking!!!!!

Umepita maeneo ya kivukoni hivi karibuni?Maeneo ya soko la ndani,kuna harufu ya ajabu ambayo haiwezi kuelezeka kiasi kwamba watu wanaofanya shughuli maeneo yale watakuwa wameathirika kiafya na kisaikolojia pia.Eneo hilo la kivukoni ambapo watu,mizigo na magari huwa yanavushwa kuelekea ng'ambo ya pili ya kigamboni na kutoka kigamboni kuja kivukoni jijini Dar Es Salaam.
Eneo hilo limezungukwa na ofisi mbalimbali za serikali ikiwemo wizara ya mipango,mahakama ya biashara n.k. Serikali inajua kuhusu swala hili?Je imechukua hatua gani kutunza soko na mazingira ya eneo hilo?Vile vile watu wanaofanya shughuli zao eneo hilo wanajua haki zao na wajibu wao?Sio kila kitu serikali itufanyie imefika kipindi tuamshe vichwa vyetu kutoka kwenye usingizi mzito na kufanya jambo la tofauti katika nchi yetu.Mimi siamini kama watu wakiamua kusimamia usafi wa eneo lile itashindikana,sitaki kuamini kuwa hakuna mamlaka inayo simamia soko hilo.Inabidi tubadilike sisi kama watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu.


No comments:

Post a Comment