Photobucket

Tuesday, March 20, 2012

Nimeibamba live!!!!!

Jengo hilo kama linavyoonekana nimelibamba maeneo ya posta karibu na hoteli ya kempiski na benki kuu ya Tanzania.Kuna maelezo tafauti tofauti juu ya hawa watu wanaojiita freemasons.Wengine wakisema ni mtandao wa watu wenye pesa ambao husaidia watu mbali mbali lakini kwa masharti kadha wa kadha.Aidha wengine wakisema ni kikundi cha wapinga Kristu na wanaabudu mashetani.
Kikundi hiki kilikuwepo nchini hata kabla ya kupata uhuru na kuzaliwa kwa Tanzania na inavyosemekana chimbiko la mataifa makubwa ya Ulaya na Marekani.
Inasemekana kundi hili hutumia watu maarufu na matajiri wanaopendwa na watu na wenye uwezo wa kushawishi watu ili wapate kuingia katika kundi hilo.Huwa na ishara zao mbalimbali ambazo hutumika kutambuana,watu mbalimbali mashughuli ikiwemo wanasiasa na wasanii wamekuwa wakionyesha ishara hizo wakiwa kwenye kundi la watu.
Baadhi ya wasanii wakubwa wa nje hususani marekani wamekuwa wakidaiwa kujihusisha na kikundi cha watu hawa yaani freemasons.Moja ya wasanii pendwa marekani bwana Jay z amekuwa akidaiwa kuwa ni mmoja wa watu hao kutokana na kuonyesha ishara mbalimbali za kundi hilo kwenye video zake au kwenye maonyesho mbalimbali mbalimbali ya kimuziki.
Kwa hapa nchini Tanzania kuna baadhi ya watu mashughuli na wanaojulikana,kuwa wanajihusisha pia na kikundi hicho cha freemasons.Kwasababu za kiusalama nisinge penda kutaja majina ya watu hao
Vijana wengi wamekuwa wakiiga baadhi ya ishara na matendo wanayofanya wasanii wakubwa wa nje pasipo kujua nini wanachokifanya.Wengine ni kwa kukosa tuu maarifa wanajikuta wakiiga mambo hayo na kujisifu.
Ndugu zangu watanzania inabidi tuwe macho kweli na hizi tamaduni tunazozigeza kutoka katika nchi za wenzetu hususani zilizo endelea.Aidha tusijefika mahala tukajilaumu kwa tunayo yafanya.Huu ni ushauri tuu unaweza kuzingatia ama usizingatie ila mwenye masikio na asikie,Ahsanteni.

No comments:

Post a Comment