Sitta kuwa mgeni rasmi mechi ya Simba dhidi ya ES Setif ya Algeria
Waziri wa jumuiya Africa mashariki Mheshimiwa Samweli Sitta atakuwa mgeni rasmi katika mechi ya kombe la shirikisho la CAF kati ya wekundu wa msimbazi Simba na timu kutoka algeria ES Setif
Bwana Ismail Aden Rage mwenyekiti wa simba alithibitisha kuwa mheshimiwa waziri wa jumiya ya Afrika Mashariki na shabiki mzuri wa simba Mh.Samwel Sitta atakuwa mgeni rasmi katika mechi itakayofanyika wiki mbili zijazo hapa nyumbani,katika uwanja wa taifa jijini Dar Es Salaam akiongezea kuwa maandalizi ya mechi hiyo ni mazuri
Es Setif itatua nchini tarehe 21 ya mwezi machi,simba ni timu pekee iliyo katika ligi ya bara,hii ni baada ya kushindwa kuondelea katika shirikisho wapinzani wao wa jadi Yanga iliyo bara vilevile na zanzibar ikiwakilishwa na Mafunzo na Jamuhuri
Timu ya Yanga ilitolewa na timu ya Misri ya Zamalek kwa kukubali ushindi wa magoli mawili kwa moja.Mafunzo ikifungwa mabao tano bila na timu ya Msumbiji Atletica Muculmano na Jamuhuli kwa kuifungwa mabao saba bila ya majibu yoyote na timu ya Zimbabwe ya Hwangwe
Simba ni tumaini la watanzania lililobaki katika mechi za shirikisho hili la Africa,Aidha aliomba watanzania kujitokeza kwa wingi na kusahau tofauti zao za kitimu.
JENGO LA MAKAO MAKUU WMA KUKABIDHIWA FEBRUARI 10, 2025, UJENZI WAFIKIA
ASILIMIA 95.2
-
Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil
Abdallah,ameridhishwa na ujenzi wa Jengo la Wakala wa Vipim...
57 minutes ago
No comments:
Post a Comment