Photobucket

Friday, April 13, 2012

Umoja ni Nguvu

Angalia vizuri picha hapo juu
Tafsiri yako ni ipi juu ya picha hiyo?
Labda ni kusaidie,
Sehemu ya juu ya picha hii inaonyesha samaki Mkubwa akitaka kumeza samaki wengi walio wadogo,ambapo wanajikuta wakikimbia pasipo eleweka.
Tuanze na mfano kwa wananchi,kuna baadhi ya wachache wanaotesa walio wengi kisa wanapesa au wana mamlaka fulani fulani,hivyo mtu mmoja anaweza kuvuruga ndoto za waliowengi,sababu ni tuu anakitu fulani kinachomlinda n.k
Tukienda kwa mfano wa nchi,Utakuta kuna Nchi fulani zenye nguvu ya pesa au majeshi inatumia mabavu yake kutesa nchi fulani fulani ziliyo nyonge,Hii inatokana na sababu mbalimbali eidha nchi hizo ndogo zina kitu fulani ambacho wakikifanikisha zitakuwa mbali kijamii,kiuchumi na kisiasa pia.Kutokana na unyonge huo na kutokuwa na umoja nchi hizo zilizo nyingi zinajikuta zikionewa na Nchi moja au chache zenye nguvu.
Vile vile kwenye upande wa biashara inawezekana kuna Kampuni moja kubwa(Monopoly) yenye masoko na pesa inatumia nafasi hiyo kukandamiza makampuni madogo madogo,kwa kukosekana kwa umoja kati yao na kushindwa biashara.
Ni machache tuu niliyojaribu kuelezea kenye sehemu ya kwanza ya Picha hii,Sasa tuelekee kwenye sehemu ya chini.
Inaonyesha yule samaki aliyekuwa anaonyesha akitaka kuwameza samaki wengine wadogo sasa samaki hao wamejiunga na ni zamu ya yule samaki mkubwa kumezwa na amejikuta kakimbia.
Fundisho ni nini??
Umoja ni nguvu utengano ni dhaifu,hivyo tunashauliwa chochote tunavyofanya inabidi tuwe na umoja hata akitokea wa kutuharibia hataweza kutushinda.
Unaweza kutoka maoni yako kwenye sanduku letu la maoni hapo chini kwa nyongeza yoyote juu ya picha hii.

No comments:

Post a Comment