Photobucket

Friday, April 27, 2012

Walijua hili????

Ni dhahiri kuwa unaifahamu sehemu hii,kwa wakazi wengi wa Dar Es Salaam wanapafahamu hapa.
Basi kama ni mgeni wa maeneo haya au eneo hili,ngoja nikuelekeze.Hii ni moja ya sehemu maarufu sana jijini Dar Es Salaam.Ambapo watu hupenda kwenda na kununua vitu mbalimbali,Kwa lugha ya kibiashara tunapaita Hyper Market,ndani kuna super market mbali mbali wanazouza vitu mbali mbali na pia kuna sehemu mbali mbali za burudani yaani Bar,movies n.k
Umeona magari mengi yalivyo egeshwa sehemu hii??
Fatana na mimi tujionee vingine
Vile vile na piki piki zimeegeshwa sehemu hii.
Tuendelee kutafiti jambo...
Eneo hili ni eneo la Taxi

Kuna fununu zimesikika kuwa Usafiri wa pikipiki za matairi matatu ali maarufu kama Bajaji haziruhusiwi kuingia eneo hili la Mlimani City...
Je,ulikuwa unalifahamu hilo??
Niliambiwa na mdau nikaenda mwenyewe kujihakikishia na bila ya mtu yoyote kujua kuwa nafanya utafiti na nikapata na majibu hapo hapo. Hasa sielewi kuwa ni kweli ama si kweli.

Pembezoni mwa Mlimani City,ni bajaj kibao zimejazana

Ni hilo tu nilitaka kukujulisha mdau wa blog hii,na kama una habari nyingine wataka kujulisha wanablogu wemgine tuandikie kupitia barua pepe yetu ya pamojatz@ymail.com
Ahsanteni kwa ushirikiano.



No comments:

Post a Comment