Photobucket

Thursday, May 10, 2012

Unalijua Hili???(Do you know this)

Ni jambo linalojulikana na wengi kuwa Tanzania ni muungano wa nchi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar.Muungano huo ulifanyika mwaka 1964-04-26 chini ya viongozi wawili Hayati Mwl.J.K Nyerere upande wa Tanganyika na Hayati Abeid Aman Karume upande wa Zanibar.

Tanzania ni nchi iliyoko Afrika ya Mashariki. Imepakana na Uganda na Kenya upande wa Kaskazini, Bahari Hindi upande wa mashariki, Msumbiji, Malawi na Zambia upande wa kusini, Kongo, Burundi na Rwanda upande wa magharibi.
Eneo lina kilometa mraba 945,203 (nchi ya 31 duniani); maji ya ndani yanachukua asilimia 6.2.
Idadi ya watu inakadiriwa (mwaka 2010) kuwa 43,188,000 (nchi ya 30 duniani) kutoka 34,443,603 waliohesabiwa katika sensa ya mwaka 2002.
Msongamano ni wa watu 46.3 kwa km2 (nchi ya 124 duniani).
Tanzania ni nchi kubwa zaidi kati ya wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Tanzania ni moja kati ya nchi maskini duniani ambazo zimefanikiwa kufutiwa madeni katika mpango wa kusamehe madeni wa Kundi la Nchi Nane.
Mji mkuu ni Dodoma, lakini makao makuu ya serikali ni bado Dar es Salaam, jiji kubwa zaidi, lenye watu zaidi ya milioni tatu. Majiji mengine ni kama vile Mwanza, Mbeya, Arusha, Tabora na Tanga.

MUUNGANO
Tangu muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 Tanzania imefuata miundo ifuatayo:
  • Nchi inatawaliwa na serikali ya muungano ikitekeleza sheria zinazotolewa na bunge la Tanzania.
  • Tanganyika au Tanzania bara haina serikali wala bunge la pekee.
  • Zanzibar (Unguja na Pemba) ina serikali na bunge lake vinavyoratibu mambo yasiyo ya muungano.
Mambo yafuatayo yalikubalika kuwa shughuli za muungano:
  • Mambo ya nje
  • Jeshi
  • Polisi
  • Mamlaka ya dharura
  • Uraia
  • Uhamiaji
  • Biashara ya nje
  • Utumishi wa umma
  • Kodi ya mapato, orodha
  • Bandari, Usafiri wa anga, Posta na Simu
DINI
Nchi haina dini rasmi na katiba ya Tanzania inatangaza uhuru wa dini kwa wote. Mara nyingi idadi ya wafuasi wa dini hutajwa kuwa theluthi moja Waislamu, theluthi moja Wakristo na theluthi moja wafuasi wa dini za jadi. Lakini tangu uhuru swali la dini ya wananchi halijaulizwa tena katika sensa, kwa hiyo kadirio la theluthi-theluthi halina msingi halisi bali ni zaidi azimio la kisiasa.
Waislamu hudai mara nyingi ya kwamba wenyewe ni sehemu kubwa ya Watanzania, angalau zaidi ya nusu. Kamusi ya "World Christian Encyclopedia" (2002) yataja Wakristo kuwa 52%, Waislamu kuwa 32% na wafuasi wa dini za jadi kuwa 14%.
Kwenye visiwa vya Zanzibar idadi ya Waislamu huaminiwa kuwa takriban 95%.

USAFIRI
Usafiri nchini Tanzania ni hasa kwa njia ya barabara. Mengine ni reli na ndege. Kwenye maziwa makubwa na pwani la Bahari Hindi kuna pia usafiri kwa meli.
Hadi sasa idadi ya barabara za lami si kubwa. Kuna hasa njia nzuri kati ya Dar es Salaam, Mbeya katika kusini-madharibi, Dodoma katika kitovu cha nchi, Arusha / Tanga katika kaskazini-mashariki. Kusini-Mashariki na Magharibi ya nchi kwa jumla haina barabara nzuri na mawasiliano ni magumu.
Shirika mbili za reli zahudumia Tanzania ni TRC (Shirika ya Reli Tanzania - Tanzania Railways Corporation) na TAZARA (Tanzania-Zambia Railways Corporation). TRC imetawala reli ya kati kuanzia Dar es Salaam hadi Kigoma halafu reli ya Tanga kati ya Tanga na Arusha. Tazara imeunganisha Dar es Salaam na kusini ya nchi hadi Zambia. Zote hazikutunzwa vizuri na usafiri unakumbwa na huduma mbaya pamoja na ajali.
Huduma kwa ndege zatumia hasa nyanja za ndege 11 penye barabara ya lami kwa ajili ya ndege hasa Julius Nyerere/Dar es Salaam, Kilimanjaro /Arusha-Moshi na Zanzibar-Kisauni.

SANAA
Kati ya wasanii wa Tanzania ni hasa wajume wa ubao na wachoraji waliojulikana kimataifa.
Uchongaji wa mabombwe ya Kimakonde yamesifiwa tangu mwanzo wa karne ya 20. Wamakonde wengi wamehamia Daressalaam au Arusha wanapohudumia soko la watalii na soko la nje.
Tangu miaka ya 1970 uchoraji wa "tingatinga" umejulikana: ulipata jina hilo kutoka kwa Edward Tingatinga naye mtu wa Umakonde.
Utamaduni wa Watanzania ni pamoja na ustaraabu  na ukarimu.Miziki aina mbalimbali hupatikana Tanzania kama muziki wa nyimbo za taraab haswa visiwani na pwani,ngoma za jadi karibia makabila yote,Mziki wa kipekee wa Bongo Flava,ambao umewateka vijana wengi,miziki ya Dansi n.k
Vile vile muziki wa Injili unakuja kasi kwa sasa nchini Tanzania huku vijana wengi wakiwa wameshikilia soko la muziki huo.

Urithi wa Dunia

Mahali pafuatapo katika Tanzania pamepokewa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia".
(mwaka wa kukubaliwa - jina la mahali)
  • 1979 – Hifadhi ya Taifa Ngorongoro
  • 1981 – Hifadhi ya Taifa la Serengeti
  • 1981 – Maghofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara
  • 1982 – Hifadhi ya Taifa Selous
  • 1987 – Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro
  • 2000 – Mji Mkongwe wa Jiji la Zanzibar / Unguja
  • 2006 - Michoro ya Kondoa
  • Tanzania ni nchi pekee Duniani inayochimbwa madini ya Tanzanite
Nb.Karibia kila kona ya Tanzania kuna mali asili,Je?IKwanini mpaka sasa haijaendelea????

No comments:

Post a Comment