Photobucket

Thursday, June 14, 2012

Dogo Janja OUT Tip Top..


Jana msanii na kiongozi wa kundi la kimuziki la Tip Top Connection Madee alifunguka na kueleza kuwa ameamua kumrudisha msanii Dogo Janja mkoani kwao Arusha kutokana na tabia alizokuwa nazo msanii huyo.
Aidha aliendelea kufunguka na kuelezea kisa kizima cha uamuzi huo kama ifuatavyo " Mimi nilikuwa nimesafiri ni kama wiki mbili zimepita tulikuwa mkoa wa Iringa na Mbeya, mimi na Tunda yaani Tip Top kwa ujumla yeye tulimbakisha kwa maana yupo kipindi cha mitihani yeye ni  form Two"

Msanii huyo aliendelea kufunguka na kueleza baada ya kurudi kwenye safari hiyo alipigiwa simu na mwalimu wa darasa wa Dogo janja na kumpa pole kwa kuumwa kwa mwanafunzi wake.
Ndipo akaamua kumpigia simu Dogo Janja bila mafanikio yoyote jambo lililomfanya ampigie msanii mwenzake wa kundi hilo aitwaye Tunda.Ambapo aliambiwa kuwa amemuacha msanii huyo nyumbani kwake.


Aidha alikubali kumchapa makofi dogo huyo na kumwambia awahi nyumbani haraka baada ya kumkuta nyumbani kwa Tunda na kesho yake anampaleka shule aka adhibiwe. Kesho yake alikaa na kuongea na msanii huyo akijiandaa ampeleke shule na ndipo msanii huyo alipokataa kwenda shule na kutaka ahamishiwe kusoma Arusha mji aliotokea.
Hivyo Madee aliamua kumpigia baba yake na Dogo janja na wakakubaliana kubaki kwa msanii huyo.

Alieleza jambo lililomuuzi zaidi ni baada ya kuchukua simu ya Dogo janja na kukuta mambo ya ajabu ikiwemo nyaraka todfauti zinazomsema madee na mambo mengine ya ajabu. Vilevile Dogo janja aligoa kabisa kwenda shule na kutaka arudi Arusha ndipo madee akatoa baraka zake zote na hivi leo asubuhi amesafiri kuelekea Arusha.

No comments:

Post a Comment